Tangaza Hapa Ad

Mix

Taarifa ya polisi kuhusu kukamatwa na polisi watu wanaolala Guest mchana DSM

on

Inawezeka uliisikia hii ya polisi kukamata watu wanaolala nyumba za kulala wageni wakati wa mchana Dar es slaam, sasa leo September imetolewa taarifa kutoka jeshi la polisi  ikitoa rai kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani kupuuza taarifa hizo.

Taarifa hiyo imedsema kuwa uvumi huo pia umechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba askari polisi wanawakamata watu ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Rais Magufuli hapa kazi tu.

Taarifa hiyo imeleza kuwa……>>>kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na operesheni za kuwaska watuhumiwa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria ‘Guest bubu’ majambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

>>>‘Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo jeshi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata’: Taarifa ya jeshi la polisi

ULIKOSA HII YA PROF. LIPUMBA KUHUSU DENI LA TAIFA, NI KILA MTANZANIA ANATAKIWA KULIPA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement