Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Polisi waongea ilivyokua mpaka wakamuachia Dr. Luis Shika leo

on

Tumemsoma sana kwenye vichwa vya habari kuanzia wiki iliyopita baada ya kwenda kwenye mnada wa nyumba za mabilioni na kushinda nafasi ya kununua nyumba 2 za zaidi ya Bilioni 2 lakini baadae akakamatwa na Polisi kwa kutokua na pesa mfukoni.

Jioni ya leo  November 14 2017 Polisi Dar es salaam imemuachia kwa dhamana Dr. Shika baada ya kumshikilia toka wiki iliyopita kwenye kituo cha Polisi kati siku kadhaa tu baada ya kusema atashughulikiwa kama Muhalifu mwingine na kufikishwa Mahakamani.

Inawezekana ukajiuliza imekuaje mpaka ameachiwa? Kamanda Mambosasa wa Kanda Maalum ya Dar es salaam amesema “Amepata dhamana…. amejidhamini mwenyewe baada ya kukosa mtu wa kumdhamini, dhamana yake ilikua wazi”

“Baada ya dhamana anatakiwa kuripoti Polisi kila siku na hata kesho utaratibu kutoka kwa Mwanasheria ukikamilika tutampeleka Mahakamani” – Kamanda Mambosasa

VIDEO: MWANZO MWISHO TAJIRI MTATA ALIVYONUNUA NYUMBA ZA BILIONI 2 WAKATI HANA KITU MFUKONI

VIDEO: IMEFAHAMIKA HIKI NDIO KIJIWE CHA DR. LUIS SHIKA ANACHOFANYIA KAZI ZAKE MARA KWA MARA… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUKITAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments