Tangaza Hapa Ad

Michezo

Habari ya The Sun iliyomkwaza Raiola kuhusu Pogba na girlfriend wake

on

England ni moja kati ya nchi ambazo wanasoka wakubwa wanaojiunga na Ligi hiyo hupata wakati mgumu kutokana na kutajwa kuwa vyombo vya habari vya England vinawafuatilia sana, moja kati ya habari zilizoingia kwenye headlines leo ni habari ya kiungo wa Man United Paul Pogba na mpenzi wake Dencia.

Pogba ambaye toka amerudi Man United bado anaishi katika hotel jijini Manchester, mpenzi wake Dencia ameandikwa na The Sun kuwa analalamikiwa na kukera majirani zake hotelini hapo, kutokana kutuhumiwa kusumbua majirani wa jengo hilo kwa kelele zake wakati akiwa anafanya mapenzi.

snip_20161018093153

Taarifa hizo ambazo zimeenea katika mitandao chanzo kikitajwa kuwa ni The Sun, zimemkera wakala wa staa huyo Mino Raiola na kusema kuwa huo ni uzushi wa gazeti hilo ambao umelenga kuuza kwa kutumia jina la mteja wake, kwa sasa Paul Pogba yupo katika mahusiano na Dencia ambaye ni muimbaji.

2a1b4bac00000578-0-image-m-9_1435660442745

Mino Raiola

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement