PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Liverpool wameondoka kibabe Wembley vs Tottenham Hotspurs

on

Moja kati ya michezo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu leo katika Ligi Kuu England ni mchezo kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Liverpool game ambayo imechezwa katika uwanja wa Wembley London ambapo unatumiwa na Tottenham kwa sasa kama uwanja wa nyumbani.

Tottenham wakiwa nyumbani wamekutana na bahati mbaya ya kupokea kipigo cha magoli 2-1, magoli ya Liverpool yakifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 39, Robert Firmino dakika ya 54 wakati goli la Tottenham likifungwa na Erik Lamela dakika tatu za nyongeza kabla ya game kuisha.

Kipigo hicho sasa kinaiweka Tottenham nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 kwa kubakia na point 9 wakati Liverpool wameendelea kuwa kileleni kwa kuwa na jumla ya point 15 baada ya kupata ushindi katika game zote tano za Ligi Kuu.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments