Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: ‘Kuna watu tumewakamata katika tukio la mauaji ya Polisi’ -Kamanda Sirro

on

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amekutana na waandishi wa habari leo August 27 2016 na kuongelea kwa ufupi taarifa za tukio la mashambulizi lililotokea Vikindu mkoa wa Pwani ambapo amesema taarifa kamili zitatolewa siku ya jumanne ikiwa ni pamoja na zile zinazodaiwa kuwa miongoni mwa wahalifu hao ni askari wastaafu.

Kamanda Sirro amesema…>>>’Siku ya jana kulikuwa na operation kule Vikindu, kuna watu wameuawa na wengine tumekwisha wakamata lakini taarifa kamili kuhusu kilichotokea tutazitoa siku ya jumanne hivyo tunaomba uvumilivu wenu katika hili

Ni lazima tusafishe Dar es salaam nzima inaendelea kuwa salama siku zote lakini pia kwa sasa siwezi kuongelea kama wahusika wa tukio la ujambazi ni miongoni mwa askari ama sivyo muda ukifika nitayaeleza yote‘ –Simon Sirro

Muda huu nimewapeleka askari wangu zaidi ya 80 katika operation ambayo itaanzia Vikindu kuelekea Pwani na maeneo mengine ya Dar es salaam‘ –Simon Sirro

ALICHOKIONGEA WAZIRI NCHEMBA BAADA YA KUFIKA ENEO WALIPOUAWA ASKARI DAR

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement