Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Prof. Kabudi aongoza kamati ya JPM katika mazungumzo na Airtel

on

Leo March 12, 2018 Mazungumzo kati ya Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel inayomiliki hisa katika kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania yameanza rasmi.

Katika mazungumzo hayo kamati iliyoundwa na Rais Magufuli inaongozwa na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na timu ya Bharti Airtel inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wake Mukesh Bhavnani.

Mazungumzo hayo yanalengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili (Serikali ya Tanzania na Bharti Airtel) na kuimarisha sekta ya mawasiliano nchini Tanzania.

Kampuni ya Bharti Airtel iliomba kufanyika kwa mazaungumzo hayo baada ya kamati iliyofanya uchunguzi kuhusu umiliki wa kampuni ya Airtel Tanzania kuwasilisha ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

“HATA WAKIANDAMANA NDANI YA NYUMBA, MTU AKAUMIA, ALIYEITISHA ATAWAJIBIKA” -WAZIRI MWIGULUSoma na hizi

Tupia Comments