Tangaza Hapa Ad

Mix

Alichokisema Mrema baada ya Mchungaji Lwakatare kuwakomboa wafungwa 78

on

Tangu wiki moja ipite kwa mchungaji wa kanisa la mlima wa moto Assemblies of God , Mikocheni ‘B’ Dr. Getrude Lwakatare kutoa milion 25 kuwalipia wafungwa ambao walikosa fedha kulipia faini na kufungwa jela, Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa Augustino Mrema amependekeza kufanyika kwa harambee kwa makanisa yote TZ.

Mrema ameomba makanisa yote kutoa sadaka za siku moja ya Jumapili ili zikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani na misikiti pia itenge ijumaa moja.

Mrema ameomba hili zoezi lifanyike kabla ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya ili wafungwa waweze kusheherekea sikukuu hizo, pia ametoa wito kwa wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima wakubwa nao wachangie kwenye kampeni hiyo ya kuwakomboa wafungwa kutoka magerezani.

ULIKOSA HII YA MREMA KUAMUA KWENDA KUMUONA RAIS MAGUFULI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement