Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Prof. Lipumba ‘sitambui maamuzi yaliyotoka Znz, bado mimi ni Mwenyekiti’

on

Kutana na maneno ya Profesa Lipumba ambaye kwenye siku za karibuni amehusika kwenye vichwa vya habari kuhusu uwanachama wake na akiendelea kuutaka uenyekiti wake na hii ni baada ya viongozi wa C.U.F kuonekana kutomtaka.

Baada ya mkutano mkuu kuharibika walipaswa kama wanakaa kikao wakae hapahapa ambapo Wajumbe wote wapo, Jumapili hii ndio wamefanya kikao Zanzibar na Wajumbe wengi wameshindwa kwenda hata Mama Magdalena Sakaya msaidizi hakushirikishwa kabisa, hivyo ni vikao vya kimafia

Tayari nilishaandika barua kwa msajili kwamba nilijiuzulu lakini baada ya ushauri wa Wanachama na viongozi kunitaka nirudi kwenye uongozi wa chama niliandika barua ya kutengua na katibu mkuu akanijibu nisianze kazi kama nilivyopanga sababu anatafuta ushauri wa kisheria‘ – Profesa Lipumba

Kwa mujibu wa ITV, Profesa Lipumba amesema ‘Mkutano wa Jumapili iliyopita ulivurugika sababu palikua na ajenda ya kupanga, sasa wamekwenda kikao wamefanyia Znz kwahiyo sitambui kabisa maamuzi yaliyotoka Znz, natambua ni mwenyekiti halali wa C.U.F na nitaanza kufanya shughuli zangu nasubiri tu kauli ya msajili wa vyama vya siasa

Msikilize zaidi Profesa Lipumba kwa kubonyeza play hapa chini….

ULIZIKOSA ZA KITWANGA KUMUUNGA MKONO MAGUFULI? SIRI ZA UKUTA KUAHIRISHWA JE? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement