PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

Michezo

Neymar akitoka kapa Messi anapiga hat-trick ya kwanza

on

Usiku wa September 18 2019 michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 ilianza rasmi kwa game nane za mwanzo za hatua ya makundi ya michuano hiyo kuchezwa, miongoni mwa game zilizochezwa usiku huo ni game kati ya FC Barcelona ya Hispania dhidi ya PSV ya Uholanzi.

Game ya FC Barcelona na PSV imechezwa katika uwanja wa nyumbani wa FC Barcelona unaojulikana kwa jina la Camp Nou, FC Barcelona wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa magoli 4-0, staa wao Lionel Messi akiwa ndio mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick katika UEFA msimu huu.

Barcelona walianza kupata goli la kwanza dakika ya 32 kupitia kwa Lionel Messi na dakika ya 74 Dembele akafunga goli la pili kabla ya Lionel Messi kukamilisha hat-trick yake kwa kufunga magoli mawili dakika ya 77 na 87, ushindi huo sasa unawafanya Barcelona kuongoza Kundi B kwa tofauti ya magoli wakifuatiwa na Inter Milan waliokuwa na point tatu kama wao ila wanatofautiana ya magoli.

Kwa upande wa Neymar akiwa na club yake ya PSG leo dhidi ya Liverpool wamejikuta wakipoteza kwa magoli 3-2 katika uwanja wa Anfield, huku Neymar akiondoka bila goli katika game hiyo ya mwanza ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 hatua ya Makundi.

Matokeo ya game zote nane za UEFA Champions League hatua ya Makundi zilizochezwa usiku wa September 18 2018.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments