BreakingNews

BREAKING NEWS: Treni ya abiria yapata ajali ikitokea Kigoma Tanzania leo Jan 29 2017

on

Treni ya abiria ya EXPRESS ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam leo January 29 2017 imepata ajali maeneo ya Ruvu ndani ya mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika kwenye jiji la Dar es salaam.

Shuhuda ambaye alikua ndani ya Treni hiyo ameongea na Perfect Crispin kwenye ON POINT ya CloudsFM na kuthibitisha kutokea kwa ajili hiyo akisema Behewa zaidi ya 10 zimepinduka na watu wanaendelea kuokolewa kwa kupitia Madirishani.

Amesema ‘Treni imepata ajali kama kilometa moja kutoka Mto Ruvu, abiria wanazidi kuokolewa na hivi ninavyoongea na wewe hatujui idadi ya waliojeruhiwa wala kufariki ni wangapi

Behewa langu ndio lilikua la mwisho kuanguka kwahiyo sisi tumenusurika kiasi, majeruhi wameumia kiukweli wamejeruhiwa sana…. wanalazwa chini na kumwagiwa maji, bado Polisi hawajafika kwenye eneo la ajali

millardayo.com na AyoTV zinaendelea kufatilia habari hii kwa Mamlaka husika ili kupata taarifa kamili ya kila kilichotokea na kinachoendelea.

ULIKOSA KUONA? Wanajeshi Makomando wa Tanzania wakionyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli? bonyeza play kwenye hii video hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments