Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Isikupite ya askari wa Congo wanavyosimamisha magari kwa kutega misumari

on

Mtu wangu wa nguvu ambaye hujawahi kufika Lubumbashi DRC Congo hii inaweza ikakushangaza kidogo, askari wa usalama wa barabarani Lubumbashi wanatumia chuma chenye vitu vyenye ncha kali kusimamisha magari barabarani ili kuyafanyia uchunguzi.

Naambiwa Lubumbashi ukimsimamisha dereva wa gari pasipo kumuwekea hivyo hawezi kusimama tofauti na kwetu Tanzania ambapo trafiki wamekuwa wakisimamisha magari kwa kupunga mkono tu bila kuweka kizuizi chochote na dereva ana heshimu na kusimama, hivyo chuma kile kinamfanya asimame bila kupenda kwa kuogopa kutoboa matairi yake.

Nimekusogezea video niliyojaribu kurekodi kwa siri mtu kukiwa na chuma chenye misumari na pikipiki ya polisi ikiwa pembeni

 Kifaa kinachotumika Restaurant za Lubumbashi kumjulisha mteja chakula chake tayari

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement