Michezo

Matokeo ya TPL, Okwi kaanza kazi leo October 6 2018

on

Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea tena leo kwa michezo mitano kuchezwa katika viwanja mbalimbali, Simba alikuwa uwanja wa Taifa kucheza dhidi ya African Lyon.

Game ya Simba uwanja wa Taifa ilifanikiwa kumalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-1, magoli ya Simba yakipatikana dakika ya 9 kupitia kwa Shiza Kichuya na Emmanuel Okwi akafunga goli la pili dakika ya 48 ya mchezo.

Takwimu za game ya Simba na African Lyon

Emmanuel Okwi ambaye ni mfungaji bora msimu uliopita, goli lake la leo ndio linakuwa goli lake la kwanza Ligi Kuu msimu huu, goli pekee la African Lyon lilifungwa na Awadh Juma dakika ya 62.

Matokeo ya game za TPL leo October 6 2018.

Msimamo wa TPL ulivyo kwa sasa.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments