Premier Bet

Top Stories

Rais Magufuli alivyowaweka kikaangoni Wakurugenzi Ikulu “mbona hamuelewi” (+video)

on

Rais John Magufuli amelijua juu Shirika la umeme nchini TANESCO kwa kushindwa kuwaunga mkono wabunifu waliobuni mtambo mdogo wa kufua umeme kwa kutumia maji ya mto Mkoani Njombe, na kuwataka kuwalipa wabaunifu hao fedha watakazozitumia kama kianzio cha kununua vifaa kwa ajili ya shughuli zao.

TANESCO hakikisheni mnaondoka na hawa waliozalisha umeme kwenda kuangalia hiyo mitambo na kuweka kinga maana mlitakiwa muwape ushirikiano kuanzia mwanzo lakini hamkufanya hivyo, na wasiondoke na basi kama walivyokuja mchukue magari yenu yenye nembo ya TANESCO” Rais Magufuli

TANESCO ndio mlitakiwa kuwasaidia hawa lakini muwakilishi wenu mliyemuweka anasema mpaka watakapokuja akiwa amekaa mwenye kiti anazunguka huku amevaa miwani meusi wakati yuko ofisini na jua hamlichomi wakati angekuwa ameshaenda pale na kuuona huo mradi,” Rais Magufuli

LIVE IKULU: RAIS MAGUFULI ANAWABANA WAKURUGENZI “WAONDOKE IKULU HIVI HIVI”

Soma na hizi

Tupia Comments