Tangaza Hapa Ad

Michezo

Maamuzi yalioafikiwa kuhusu refa aliyechezesha mechi ya Yanga na Simba

on

Katika soka la bongo kwa sasa habari inayosambaa kwa kiasi kikubwa mtandaoni ni kuhusiana na muamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya Yanga na Simba October 1 2016 na line one Samwel Mpenzu kufungiwa miaka miwili, bado TFF hajatangaza rasmi adhabu hiyo lakini taarifa zilizoenea mitandaoni ni hizo na TFF hawajakanusha.

Kuna habari kuwa muamzi Martin Saanya na msaidizi wake Samuel Mpenzu wamefungiwa miaka miwili kuchezesha soka, lakini pia inaripotiwa kuwa kadi nyekundu aliooneshwa nahodha wa Simba Jonas Mkude imefutwa, hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli ya 1-1.

Maamuzi hayo yanatajwa kufikiwa baada ya kamati ya saa 72 kukaa na kupitia malalamiko kuhusu refa kulikubali goli la mkono la Amissi Tambwe na line one Samwel Mpenzu kulikataa goli la Ibrahim Ajib kwa kusema kuwa aliotea.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement