Tangaza Hapa Ad

Michezo

Staa wa Liverpool anaeripotiwa kuwa ataondoka mwezi January

on

Bado zaidi ya mwezi dirisha dogo la usajili la mwezi January kwa barani Ulaya lifunguliwe, tayari majina ya baadhi wachezaji yameshaanza kutajwa kutaka kuhama klabu moja na kujiunga na nyingine.

Kwa upande wa beki wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea Liverpool Mamadou Sakho anaripotiwa kutaka kuondoka Liverpool mwezi January, anaweza akahama kabisa Ligi Kuu England.

mamadou-sakho

Liverpool Echo wameripoti kuwa klabu ya West Brom imeonesha nia ya kumchukua beki huyo, lakini ni kwa mkopo na wala sio mkataba wa moja kwa moja.

Sakho ambaye alikuwa beki chaguo la kwanza wa klabu ya Liverpool hadi mwezi April, amepoteza nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza toka afungiwe kwa kudaiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement