Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Msimamo wa Azam FC kuhusu uwanja gani watacheza na Simba SC

on

Baada ya klabu ya Azam FC kuandika barua na kuonesha msimamo wao kuhusu kuiomba TFF kutocheza baadhi ya mechi zao za nyumbani zinazohusisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa kama wa nyumbani na kutaka kutumia uwanja wao wa Chamazi Complex.

Kuelekea mchezo dhidi ya Simba afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ameweka wazi msimamo wao kuhusu mchezo wao dhidi ya Simba kuwa hawatacheza uwanja wa Taifa na badala yake watacheza uwanja wa Chamazi.

“Kikukweli hatuoni sababu yoyote ya kutocheza mechi zetu zote uwanja wa wetu wa Chamazi, kwa sababu umesajiliwa na CAF, sisi msimamo wetu uko pale pale mchezo wetu dhidi ya Simba utachezwa Chamazi vinginevyo labda kama utakuwa wamebadilisha na umekuwa wa ugenini”

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement