Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Togo wameondolewa AFCON 2017 kwa kipigo cha goli 3-1 kutoka DR Congo

on

Timu ya taifa ya Togo ikiongozwa na nahodha wao Emmanuel Adebayor usiku wa January 24 imejikuta ikiondolewa katika michuano ya AFCON 2017 kufuatia kipigo cha goli 3-1 katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C wa AFCON 2017.

Togo ambao walikuwa wanahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya safari yao ya kucheza robo fainali ya AFCON 2017, magoli ya Junior Kabananga dakika ya 29, Firmin Mubele dakika ya 54 na Paul M’poku dakika ya 80 yamewafanya ndoto yao ya kucheza hatua ya robo fainali kushindikana na kuambulia goli moja lililofungwa na Laba Kodjo dakika ya 69.

Timu ya taifa ya Togo imeaga michuano hiyo ikiishia hatua ya makundi na kumaliza ikiwa mkiani kwa kuwa na point 1 katika Kundi C, ambalo timu za DR Congo na Morocco ndio zimefuzu kucheza robo fainali ya AFCON 2017.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement