Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya kuifunga mara 6 katika mechi 7, Yanga imelazimishwa sare na African Lyon

on

Ligi Kuu Soka Tanzania bara imeendelea leo December 23 2016 kwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Dar es Salaam Young Africans kucheza dhidi ya African Lyon katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kabla ya mchezo wa leo African Lyon kucheza na Yanga, rekodi zilikuwa zinasomeka kuwa kwa mechi 7 zilizopita, African Lyon hajawahi kumfunga Yanga huku akiwa amekubali kufungwa mara sita na kutoa sare mechi moja pekee toka tarehe 27/10/2010.

img-20161223-wa0050

Yanga leo wameshindwa kutamba mbele ya African Lyon na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1, Venance Ludovic ndio aliipatia goli la kwanza African Lyon dakika ya 59, kabla ya Amissi Tambwe kuisawazishia Yanga goli dakika ya 74.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement