Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kauli ya kocha wa Argentina baada ya maneno kuzidi kuwa Messi anamchagulia wachezaji

on

Moja kati ya vipindi vigumu kwa staa wa soka wa kimataifa wa Argentina anayeichezea FC Barcelona Lionel Messi ni kipindi hiki ambacho Argentina haifanyi vizuri sana, Lionel Messi ambaye ni nahodha wa Argentina aliwahi kulaumiwa na kuandikwa kuwa hajitumi timu ya taifa.

Lionel Messi pia amewahi kutuhumiwa kuwa amekuwa na sauti katika uchaguzi wa wachezaji wa timu ya taifa mbele ya kocha wao Edgardo Bauza madai ambayo kocha Bauza amekuwa akiyapuuzia na kukaa kimya.

lavanguardia_g_874703504-k7ub-u301455491366e5b-992x558lavanguardia-web

Maxi Lopez kushoto akiwa na Lionel Messi wakati wakiwa FC Barcelona

Kocha Bauza ameamua kuzungumzia kuhusiana na maneno hayo “Kwa wale wanaofikiria kuwa Lionel Messi anachagua wachezaji wa kuunda kikosi cha timu ya taifa, sidhani kama kuna haja ya kuwajibu, kama Messi akichagua wachezaji basi nitakuwa nje ya timu”

Kama utakuwa unakumbuka October 14 Lionel Messi alidaiwa kuhusika na kuzuia mchezaji Mauro Icardi asiitwe timu ya taifa, kwa sababu alimchukua mke wa mchezaji mwenzake wa Argentina na rafiki yake ambaye amewahi kucheza nae FC Barcelona Maxi Lopez.

0012709961

Mauro Icardi akitoka na Maxi Lopez akiingia hii ilikuwa wakati wanachezao wote Sampdoria

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement