Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya kipigo mechi ya kwanza, Jang’ombe Boys imewaadhibu Mabingwa watetezi leo

on

Michuano ya 11 ya Kombe la Mapinduzi 2017 bado inaendelea visiwani Zanzibar kwa timu tisa kuwania taji hilo, leo January 3 2017 ilikuwa ni zamu ya michezo ya pili ya Kundi A, mchezo wa kwanza kwa leo January 3 2017 ulikuwa unazikutanisha timu za Jang’ombe Boys dhidi ya URA ya Uganda.

img-20170103-wa0001

Baada ya Jang’ombe Boys kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya wapinzani wao wakuu kwa hapa Unguja Taifa Jang’ombe, leo January 3 2016 wamekuwa wababe wa mabingwa watetezi wa michuano hiyo URA.

img-20170103-wa0002

Jang’ombe Boys wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ambayo yalipatika kupitia Hamisi Mussa Rais dakika ya 16 na 30, wakati kwa URA wamepata goli kwa kupitia Lapama Bogota dakika ya 23 na kufikisha jumla ya goli 3 katika michuano ya Mapinduzi Cup 2017.

img-20170103-wa0003

Matokeo hayo yanalifanya Kundi A kuwa kila timu kuwa na matumaini ya kusonga mbele, kutokana na kila timu hadi sasa ina point 3 kasoro KVZ ambao watacheza dhidi ya Simba wenye point tatu pia saa 20:30 katika uwanja wa Amaan.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement