Tangaza Hapa Ad

Michezo

Dortmund imemsajili Isak anayetabiriwa kuwa kama Zlatan Ibrahimovic

on

Club ya soka ya Borussia Dortmund ya Ujerumani imefanikiwa kuishinda Real Madrid katika mbio za kuwania saini ya kinda mahiri kutoka Sweden Alexander Isak.

Alexander Isak mwenye umri wa miaka 17 amesajiliwa na Borussia Dortmund akitabiriwa kuja kuwa na umahiri kama mkongwe wa Sweden anayeichezea Man United Zlatan Ibrahimovic,

Isak anaripotiwa kusajiliwa kwa dau la pound milioni 8.6 na mkataba wake japo haijatajwa ni wa miaka mingapi, imeripotiwa ni wa muda mrefu.

Gazeti la Marca la Hispania liliripoti kuwa staa huyo aliyekuwa asajiliwe na Real Madrid mwishoni mwa wiki hii kwa dau la pound 8.6, anatajwa kuwa ndio mchezaji ghali zaidi kinda kwa Sweden kusajiliwa baada ya Zlatan Ibrahimovic kusajiliwa na Ajax 2001 akitokea Malmo kwa pound 7.5.

Rekodi za Isack akiwa katika timu ya AIK

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement