Tangaza Hapa Ad

Michezo

Staa wa Genk atakayejiunga na Leicester January 1, mashabiki wameanza kumuaga

on

Taarifa ambayo imeenea katika mitandao ya kijamii na baadhi ya mitandao ya habari za michezo ya England ni kuhusiana na kiungo wa kimataifa wa Nigeria anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji Wilfred Ndindi kuripotiwa kukaribia kujiunga na Leicester City January 1 2017.

wildred-ndidi-leicester-city-transfer-done-deal-747618

Stori kutoka express.co.uk inaripotiwa kuwa Ndindi tayari amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Leicester City kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi January 1 2017, Ndindi anajiunga na Leicester City kwa dau la pound milioni 15, Ndindi amecheza jumla ya mechi 33 akiwa na Genk na kufunga goli 3, Ndindi atakuwa mbadala wa Ng’olo Kante aliyejiunga na Chelsea.

wilfred-ndidi-leicester-city-transfer-done-deal-769329

Mtu wa karibu na Ndindi amenukuliwa na express.co.uk kuwa Ndindi kacheza mchezo wa mwisho akiwa na Genk dhidi ya KAA Gent na atasafiri January 1 kwenda kufanya vipimo, habari ambazo zinapata uzito kutokana na baadhi ya mashabiki wa Genk instagram wameanza kumuaga, Ndindi pia alikuwa anahitajika na Man United.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement