Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Fainali ya AFCON 2017 ni Misri vs Cameroon, bye bye Ghana

on

Timu ya taifa ya Ghana usiku wa February 2 2017 inaungana na timu ya taifa ya Burkinafaso kuiga michuano ya AFCON 2017, hiyo inatokana na kukubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Cameroon katika mchezo wao wa nusu fainali ya pili ya AFCON.

Ghana ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa na mashabiki wengi wa soka kuwa wanaweza kufanya vizuri zaidi katika mchezo huo wa nusu fainali na kuingia fainali, walijikuta wakiruhusu kufungwa dakika ya 72 ya mchezo na dakika za nyongeza wakiwa wanahangaika kusawazisha walifungwa goli la pili kwa shambulizi la kushitukiza.

Magoli ya Cameroon yalifungwa na Michael Ngadeu dakika ya 72 kabla ya Christian Bassogog kuzima ndoto za Ghana kucheza fainali dakika za nyongeza, ushindi huo unaifanya Cameroon kutinga fainali ya AFCON 2017 na watacheza na fainali dhidi ya Misri, fainali ambayo itakuwa inajirudia ya mwaka 2008 ambapo Misri alimfunga Cameroon na kutwaa taji lake la sita.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement