Tangaza Hapa Ad

Michezo

KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta, imemfuta kazi kocha wake

on

Timu ya KRC Genk ya Ubelgiji leo kupitia tovuti rasmi ya timu hiyo imetangaza kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake mkuu Peter Maes kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo kwa mechi za hivi karibuni.

Peter Maes anafutwa kazi ikiwa imebakia siku moja kabla ya KRC Genk kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KAA Gent utakaochezwa kesho December 27 katika uwanja wa nyumbani wa Genk Luminus Arena.

peter-maes

Peter Maes

Uongozi wa KRC Genk umefikia maamuzi hayo ikiwa Peter Maes amedumu katika timu hiyo toka mwaka 2015, Maes mwenye umri wa miaka 52 alijiunga na KRC Genk mwaka 2015 akitokea timu ya Lokeren inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji pia.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement