Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba imelazimishwa sare tasa na Mtibwa Sugar

on

Wekundu wa Msimbazi Simba leo January 18 2017 ilisafiri hadi uwanja wa Jamhuri Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani kucheza mchezo wao wa 19 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.

Simba wameshuka katika uwanja wa Jamhuri Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar na kujikuta wakikabiliwa na wakati mgumu na kulazimishwa sare tasa, sare dhidi ya Mtibwa imewafanya Simba kusogelewa kwa karibu na Yanga wenye point 43 huku Simba wakiwa na point 45 katika msimamo wa VPL.

Matokeo hayo yameifanya Simba kuendelea kuwa kileleni wakifuatiwa na watani zao Yanga ambao jana walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Majimaji, ila kwa sasa Simba wamepunguza tofauti ya point na Yanga na sasa wameizidi Yanga kwa tofauti ya point mbili pekee baada ya sare dhidi ya Mtibwa.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement