Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Paul Pogba vs Florentin Pogba, Zlatan kamsaidia Paul kumfunga kaka yake

on

Usiku wa February 16 ulikuwa ni usiku wa kihistoria katika familia ya mchezaji ghali zaidi dunia Paul Pogba ambapo kwa mara ya kwanza aliingia uwanjani katika mchezo wa UEFA Europa League kucheza dhidi ya kaka yake wa damu Florentin Pogba ndani ya uwanja wa Old Trafford.

Huu ni mchezo ambao Paul Pogba alikuwa akiichezea Man United wakati Florentin Pogba akiichezea St Etienne, kivutio cha mchezo huo kilikuwa ni kwa mama na kaka wa ndugu hao Mathias Pogba ambaye aliamua kutengeneza jezi maalum nusu St Etienne na nusu Man United kuonesha upendo kwa ndugu zake wote bila upendeleo.

Katika game hiyo Man United walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0, shukrani pekee ziende kwa Zlatan Ibrahimovic aliyepiga hat-trick katika game hiyo, wakati Paul Pogba akiishia kugongesha post dakika ya 69 ya mchezo, magoli ya Zlatan yanamfanya aweke rekodi ya kuifunga St Etienne kwa mara ya 17 katika michezo 14 aliyocheza dhidi yake.

Paul Pogba na Florentin Pogba

Kwa upande wa familia ya Pogba ambapo Mourinho siku moja kabla ya game alisema kuwa anajua mama yao na Pogba ataomba game iishe kwa sare, ameshuhudia mtoto wake mmoja akiondoka na furaha mwingine majonzi, kama ufahamu Paul Pogba ana makaka wawil ambao pia wanacheza soka na ni mapacha Florentin Pogba aliyecheza dhidi yake leo na Mathias Pogba anayecheza Sparta.

FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement