Tangaza Hapa Ad

Michezo

Kabla ya Marseille Evra aliongea na Mourinho arudi Man U, kaeleza kilichotokea

on

Beki wa kimataifa wa Ufaransa ambaye amewahi kuichezea Man United kwa miaka nane kabla ya mwaka 2014 kuamua kujiunga na Juventus ya Italia Patrice Evra ameongea na Sky Sports Italia na kusema aliongea na Jose Mourinho ili arudi Man United.

Evra ameeleza kuwa alikuwa na mpango wa kurudi Man United na aliongea na kocha wa Man United Jose Mourinho lakini inaonekana kama kuna mtu ambaye Evra anasema alizuia uhamisho  wake lakini amegoma kumtaja.

“Nilikuwa nakaribia kurudi Man United na nilikuwa tayari nimeshazungumza na Mourinho lakini inaonekana kuna mtu ambaye siwezi kumtaja jina hakupenda kurudi kwangu United, hata mashabiki walikuwa na shauku na hilo lakini kwa sababu niliona klabu isingefanya chochote nikamwambia wakala wangu atafute timu nyingine”

Baada ya kusajiliwa na Marseille January 2017

“Lakini fasta Marseille wakafanikiwa kunisajili na kuniweka katika mipango yao, tulitumia kama siku moja tu kukamilisha dili hilo, kiukweli walinipokea kama MUNGU wacha niweke wazi walikuwa na uhitaji mkubwa na mimi”  – Evra

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement