Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Simba imejichukulia point 3 na magoli 3-0 vs Majimaji FC Songea

on

February 4 2017 Simba walikuwa Songea kucheza dhidi ya Majimaji FC katika muendelezo wa michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania bara, Simba ambao mchezo wao wa mwisho walifungwa goli 1-0 dhidi ya Azam FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo wamerekebisha makosa na kushinda goli  3-0 dhidi ya Majimaji FC.

Simba wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na mshambuliaji wao Ibrahim Ajib dakika ya 19, kiungo Said Hamis Ndemla dakika ya 63 na mshambuliaji wao wa kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo akafunga goli la mwisho dakika ya 88 ya mchezo.

Ushindi huo unaifanya Simba kuendelea kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Tanzania bara msimu wa 2016/2017, hivyo kwa sasa Simba na Yanga wanaoongoza Ligi Kuu wanatofautiana kwa point moja, Simba wakiwa na point 48 huku Yanga wakiwa na point 49.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments