Tangaza Hapa Ad

Michezo

Barua ya Jerry Muro kwa TFF baada ya kutumikia adhabu yake miezi 6

on

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Dar es Salaam Young Africans, leo January 5 2017 ameandika barua kwenda kwa shirikisho la soka Tanzania TFF kuomba kupunguziwa adhabu yake aliyofungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.

Jerry Muro alifungiwa na kamati ya maadili July 7 2016 kwa makosa mawili, moja alilifanya mwaka 2015 la kukaidi kulipa faini ya Tsh milioni 5 iliyoamuliwa kulipa na kamati ya nidhamu baada ya kufanya makosa na ndio kosa ambalo limemfanya afungiwe mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh Milioni 3.

screen-shot-2017-01-05-at-5-16-13-pmMaamuzi hayo ya Jerry Muro yanakuja ikiwa siku 11 zimepita toka mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kuandika ujumbe wa wazi kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi kumuombe Jerry apunguziwe adhabu hiyo ambayo ameshaitumikia miezi sita tayari.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement