Tangaza Hapa Ad

Michezo

Msiba mwingine kwenye soka Tanzania, Bonny katutangulia

on

February 17 2017 taifa la Tanzania liliamka na kupokea habari za majonzi kuhusiana na kiungo wa zamani wa timu ya Dar es Salaam Young Africans na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Godfrey Bonny ambaye alikuwa anaumwa kwa muda mrefu.

Godfrey Bonny ambaye wengi walimfahamu kupitia Yanga na kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mara kadhaa chini ya kocha Mbrazil Marcio Maximo, amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwao Mbeya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Godfrey Bonny wa pili kutoka kulia

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Godfrey Bonny alizaliwa mwaka 1980 na amewahi kuzichezea timu ya Tanzania Prisons aliyokuwa anaichezea wakati yupo Jeshi la Askari magereza kabla kuamua kujiunga na Yanga na kuachana na kazi ya Magereza.

FULL HD: All goals N’gaya vs Yanga February 12 2017, Full Time 1-5

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement