Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Yusuph Manji alivyotolewa Hospitali na kupelekwa mahakamani leo

on

Alhamisi ya February 16 mfanyabishara na mwenyekiti wa Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji alipelekwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa shitaka lake linalomkabili la kudaiwa kutumia dawa za kulevya.

Manji alifikishwa mahakamani hapo akitokea hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa kalazwa katika taasisi ya Jakaya Kikwete inayohusika na tiba za moyo, Manji amesomewa shitaka hilo na kukana na kesi yake imeahirishwa hadi March 16 2017.

Hata hivyo Manji kwa sasa ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana, ambapo hakimu alimtaka ajidhamini mwenyewe kwa Tsh milioni 10 na mdhamini mmoja ambaye ataweka dhamana ya Tsh milioni 10 ambapo katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa alijitokeza na kumdhamini.

Ulikosa hii ya Yusuph Manji baada ya kutajwa na Makonda sakata la dawa za kulevya, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement