Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mchezaji wa Leicester City aliekataa kuchezea tena kisa kocha amemsaliti

on

Staa wa soka wa timu ya soka ya Leicester City  Jose Leonardo Ulloa amerudi kwenye headlines baada ya kuonyesha kukasirishwa na kocha wake Claudio Ranieri kukiuka makubaliano yao na kusema hawezi kuichezea tena Leicester sababu Ranieri kamsaliti.

Jose Leonardo Ulloa ameeleza kuwa Ranieri alisema atamruhusu kuondoka Leicester City na kwenda kujiunga na klabu nyingine endapo itakuja mezani ofa ya kuanzia pound milioni 4 na kuendelea, cha kushangaza kocha huyo hataki kuona nyota huyo akiondoka tena.

Kocha wiki mbili zilizopita alisema kuwa kama ofa ya kati ya pound milioni 4 hadi 5 itakuja mezani ataniruhusu kuondoka lakini ninachokifahamu nikuwa ofa zilizokuja ni za kiwango hicho na zaidi lakini anazipotezea

Tweet ya Jose Leonardo kwa mashabiki wa Leicester City

Leo hii ananiambia anataka mimi niendelee kuichezea Leicester City sielewi kwa nini hataki nikaendeleze maisha yangu ya soka sehemu nyingine, kiukweli kama nitaendelea kubakia Leicester City itaathiri timu na soka langu kwa ujumla wanajua hatoendelea kunitumia lakini sijui kwa nini hawataki niondoke”

Timu ya Sunderland inamuwania nyota huyo na ipo tayari kutoa pound milioni 7 kwa ajili yake……… Sunderland wapo nafasi ya mwisho katika msimamo wa EPL huku Leicester City wakiwa nafasi ya 15 ambapo kama unakumbuka Jose Leonardo Ulloa alijiunga na Leicester 2014, kaichezea jumla ya mechi 89 na kuifungia magoli 20.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement