Tangaza Hapa Ad

Michezo

TFF imeamua kumshitaki Haji Manara wa Simba

on

Siku tatu baada ya mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kufanya mkutano na waandishi wa habari na kulituhumu shirikisho la soka Tanzania TFF kuihujumu Simba kutokana na kuchelewesha na kuingilia maamuzi ya bodi ya Ligi kuhusu Simba kupewa point 3 dhidi ya Kagera.

Leo shirikisho la soka Tanzania TFF limetoa press release ya kumpeleka katika kamati ya maadili kutokana na Haji Manara kutuhumiwa kutumia maneno ya ukali na kukiuka taratibu za soka wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari April 19 2017.

Baada ya TFF kufikia maamuzi hayo kwa mujibu wa taratibu na kanuni Haji Manara atapangiwa siku ya kuitwa mbele ya kamati ya maadili na kutoa tuhuma hizo mbele ya kamati hiyo.

VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement