Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya kufungana kwa rekodi na Ndanda FC kwa michezo mitano, leo Yanga imepata ushindi

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 28 kwa Dar es Salaam Young Africans kuendelea na harakati zake za kutetea taji lake la Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa kuikaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

img-20161228-wa0051

Yanga ambao wamekuwa na rekodi sawa na Ndanda FC kwa mechi 5 zilizopita, Yanga alikuwa kamfunga Ndanda mara moja na kufungwa mara moja huku wakiwa wametoka sare michezo mitatu, ila leo Yanga amefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0, magoli yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4 na 21, Amissi Tambwe dakika ya 25 na Vincent Bossou.

img-20161228-wa0052

Mara ya mwisho Yanga kucheza na Ndanda FC ilikuwa ni September 7 2016 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara na mchezo ulimalizika kwa suluhu ya 0-0, kwa maana hiyo Yanga na Ndanda FC wamekutana mara 6, Yanga kapata ushindi mara mbili, kafungwa mara moja na sare tatu.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement