Tangaza Hapa Ad

Michezo

Adhabu waliompa Man United shabiki wao kwa kujaribu kuuza tiketi online

on

Moja kati ya headlines zilizoingia katika soka ni kuhusiana na klabu ya Man United kutangaza adhabu kwa shabiki wake ambaye alijaribu kuuza tiketi ya mchezo wa Man United dhidi ya Fenerbahce online, shabiki wa Man United alijaribu kuuza tiketi yake ya mchezo wa ugenini.

Kama utakuwa unakumbuka mwanzoni mwa msimi Man United walitangaza kuwa kuuza tiketi ambayo tayari ulishauziwa kwa mtu mwingine ni kosa na ikitokea shabiki akafanya kosa hilo atafungiwa kuhudhuria mechi za Man United za nyumbani na ugenini kwa miaka mitatu.

screen-shot-2016-11-18-at-1-23-05-pm

“Kufuatia mchezo wetu wa ugenini dhidi ya Fenerbahce tiketi iliyokuwa imesajiliwa kwa jina lako kutangaza kuiuza kupitia mitandao ya kijamii ni kosa, kwa mujibu wa masharti utafungiwa miaka mitatu kuhudhuria mechi zetu na kufutiwa tiketi yako ya msimu pasipo kulipwa fidia”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement