Tangaza Hapa Ad

Michezo

FC Barcelona wamelazimishwa sare Nou Camp na Atletico Madrid

on

Usiku wa Septemba 21 2016 michezo ya Ligi Kuu Hispania iliendelea kama kawaida, moja kati ya mchezo uliochezwa usiku wa Septemba 21 na kuvuta hisia za mashabiki wengi ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa katika dimba la Nou Camp.

4500

Katika mchezo huo ambao mchezaji tegemezi wa FC Barcelona Lionel Messi alitolewa nje dakika ya 51 baada ya kuumia, mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kulazimishwa sare ya goli 1-1, Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 41 kupitia kwa Ivan Rakitic na baadae Atletico Madrid wakasawazisha dakika ya 61 kupitia kwa Angel Correa.

3650

FC Barcelona ambao walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 70 kufuatia matokeo sasa wanakuwa nafasi ya tatu kwa kufikisha jumla ya point 10, wakati Atletico wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point 11 na Real Madrid wanaongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 13.

Matokeo ya mechi za Laliga zilizochezwa Septemba 21 2016

  • Real Sociedad 4-1 Las Palmas
  • Granada 1-2 Athletic 
  • Real Madrid 1-1 Villarreal
  • Celta 2-1 Sporting

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement