Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Goli la kwanza la Ngassa akicheza Fanja FC ya Oman kwa mara ya kwanza

on

Winga wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka katika klabu ya Fanja FC ya Oman Mrisho Ngassa amefanikiwa kuanza maisha yake mapya ya soka katika klabu hiyo kwa kufunga goli akicheza mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo.

Ngassa ambaye amejiunga na Fanja FC akiungana na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Danny Lyanga amefunga goli katika mchezo dhidi ya Al-Nahda, mchezo ambao umemalizika kwa sare ya kufungana goli 2-2.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ngassa alijiunga na Fanja FC kwa mkataba wa miaka miwili siku 27 baada ya kuvunja mkataba wa miaka minne akiwa katumikia mwaka mmoja na klabu ya Free State ya Afrika Kusini.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement