Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Tanzania yapoteza kwa mara 6 dhidi ya Zimbabwe

on

November 13 2016 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa mgeni wa timu ya taifa ya Zimbabwe Warriors katika uwanja wa Zimbabwe National Sports, Zimbabwe ambao wanajiandaa na AFCON 2017 nchini Gabon walicheza na Tanzania wakiwa wameita kikosi cha kamili kwa ajili ya mchezo huo uliokuwa katika kalenda ya FIFA.

img_0533

Tanzania wakiwa chini ya kocha wao mkuu Charles Boniface Mkwasa na nahodha wao Mbwana Samatta walikubali kupoteza kwa jumla ya goli 3-0, Zimbabwe ambao waliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa walipata goli la kwanza dakika ya 9 kupitia kwa mshambuliaji wao anayecheza KV Oostende ya Ubelgiji Knowledge Musona.

img_0525

Mchezo ulienda mapumziko Zimbabwe wakiwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Zimbabwe wakarudi na mpango mpya uliowasaidia kufunga magoli mawili dakika ya 54 kupitia kwa Mathew Rusike na Nyasha Mushekwi dakika ya 57.

img_0561

Zimbabwe wanaonekana kuwa imara zaidi ya Tanzania kwani wapo nafasi ya 110 katika viwango vya FIFA na Tanzania wapo nafasi ya 144, kwa mechi 12 zilizopita Tanzania alikuwa kapoteza mechi 5 huku akisha mechi 2 na kutoka suluhu mechi 5.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement