Tangaza Hapa Ad

Michezo

TP Mazembe wamethibitisha Ulimwengu kumaliza mkataba na msimamo wake

on

Klabu ya TP Mazembe ya Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo October 23 2016 ilitangaza rasmi kupitia tovuti ya klabu hiyo kuwa mtanzania Thomas Ulimwengu amemaliza mkataba na TP Mazembe, lakini Ulimwengu hajataka kuongeza mkataba mwingine.

TP Mazembe kupitia tovuti yao wameeleza kuwa Ulimwengu amemaliza mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu hiyo, lakini wameweka wazi kuwa walimuhitaji lakini Ulimwengu amekataa kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na anataka kuondoka.

mazembe

Taarifa iliyoandikwa na tovuti rasmi ya klabu hiyo

Mapema mwaka huu Thomas Ulimwengu aliongea na AyoTV kutoka Lubumbashi na kuweka wazi kuwa anamalizana na TP Mazembe mwishoni mwa mwaka huu, hivyo kwa sasa malengo yake ni kufuata nyayo za rafiki yake Mbwana Samatta kwenda kucheza soka Ulaya.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement