Tangaza Hapa Ad

Michezo

Sio mke wa Wayne Rooney pekee aliyekasirishwa, hata John Terry pia

on

Bado jina la  Wayne Rooney linazidi kutawala katika social network, ikiwa saa chache tu zimepita toka mkewe Coleen Rooney aandike kuoneshwa kusikitishwa kwake kupitia account yake ya twitter kutokana na tukio la weekend kuzomewa kwa mmewe Wayne Rooney katika mchezo wa England dhidi ya Malta.

Mashabiki waliokuwa wamejitokeza katika uwanja wa Wembley walimzomea Wayne Rooney katika mchezo huo uliomalizika kwa England kuondoka na ushindi wa goli 2-0, nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry ni moja kati ya watu ambao hawakufurahishwa na kitendo kile na ametumia ukurasa wake wa instagram kuoneshwa kusikitishwa kwake.

“Rooney mfungaji bora wa England wa muda wote katika historia na hivi karibuni atakuwa moja kati ya manahodha bora waliowahi kuiongoza England, moja kati ya wachezaji bora ambao nimewahi kuwaona na furaha kucheza pamoja nao, bado ni LEGEND wa Everton, Man United, England na dunia ya mpira kwa ujumla, anatakiwa kuheshimiwa sana huyu mtu”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement