Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Matano ya kufahamu kutoka kwa Rose Muhando leo pamoja na hii video aliyoifanya Afrika Kusini.

on

Rose Muhando 31. Toka ameingia mkataba wa kuwa chini ya kampuni ya Sony miaka miwili iliyopita, hii ndio itakua single yake ya kwanza ambapo anasema ‘unaitwa Yesu Kung’uta ila mimi najua kila mtu atauita Wololo kwa sababu ndio kibwagizo kinachoanza na wimbo vizuri’

2. Single hii ilirekodiwa July 2013 South Africa lakini ilichelewa kutoka sababu ilibidi amalizie kufanya video kama ilivyotakiwa, audio isingewezekana kutoka bila video kuwa imekamilika kwa sababu ya taratibu za kiofisi.

3. Video zote mbili mpya ikiwemo hii ya ‘Wololo’ zimefanyika nchini Afrika Kusini.

4. Rose anasema ‘utofauti wa kufanya kazi na Sony ni kwamba vitu vingi sifanyi mwenyewe, ninachofanya ni kuandaa nyimbo zangu ila vingine sijui nitavaa nguo gani, nitapanda gari au ndege gani… kila kitu ni wao’

5. ‘Baada ya mimi kuanza kufanya kazi na Sony wengi wanafurahi kwamba niko hapa, wako wasiofurahi pia ila hiyo sijali… Mungu akisema imeandikwa nitafanya kama ilivyoandikwa…. Mungu akiniambia fanya ninafanya haijalishi kuna mtu anataka au kuna mtu hataki’ – Rose Muhando

Tupia Comments

Advertisement