Top Stories

HEKEHEKA: Boss Mchina awaamuru Mbwa wamng’ate mfanyakazi wake

on

Hekaheka ya Clouds Fm leo January 4, 2017 inamuhusu Kijana ambaye alikuwa akifanya kazi kwa mchina mwenyeji wa Singida anadai kuwa alisakiziwa mbwa na bosi wake ambaye ni Mchina, Mbwa hao walikuwa wanne lakini watatu ndiyo waliomjeruhi na wakati wa tukio hilo hakukuwa na mtu wa kumsaidia.

Kijana huyo anadai wakati mbwa watatu walipokuwa wakimshambulia alitokea Mbwa mkubwa akamsaidia kuzuia  mbwa wengine wasimjeruhi, baada ya kung’atwa na kushindwa kuinuka ndipo boss wake mchina alimchukua na kumpeleka polisi kisha kumpeleka hospitial japo kwa sasa kijana huyo anasema boss huyo hamuhudumii na wala hampii hela ya kula licha ya majerahaa aliyoyapata.

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza FULL STORY..

HEKAHEKA: Kilichomkuta mwanamke aliyemkata mtoto wa jirani na WEMBE

Soma na hizi

Tupia Comments