Tangaza Hapa Ad

Mix

RC Makonda atangaza mapya kuhusu biashara ya dawa za kulevya DSM

on

Leo February 2, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa ya uchunguzi wake kuhusu biashara ya dawa za kulevya kwenye jiji la Dar es salaam na kuwataja Askari Polisi 9 wanaotuhumiwa kuhusika au kujihusisha na wafanyabiashara wa dawa hizo.

RC Makonda amezitaka mamlaka za kijeshi kuwaweka chini ya ulinzi askari hao kwa mamlaka yake ili waweze kutoa taarifa kwanini dawa za kulevya bado zinaendelea kuwepo.

Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Wamiliki wake wamepewa vibali vya kufanya biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza dawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi kesho saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.

 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement