Tangaza Hapa Ad

AyoTV

AUDIO: Majibu ya RC Makonda kuhusu kauli zake zilizoibua maswali

on

Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kudai mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa alitaka kuhongwa na wafanyabiashara wa shisha huku akiwatuhumu vigogo wa jeshi la polisi, leo Gazeti la mwananchi limetoka na kichwa cha habari ‘kauli za Makonda zaibua maswali 5’ 

Moja ya swali lililoandikwa kwenye Gazeti la mwananchi ni pamoja na kwa nini RC Makonda hakuwahi kuwapa maelekezo Kamanda Sirro na Kamanda Kaganda hukohuko badala ya kuwachongea kwa Waziri mkuu? basi kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Leo November 18 2016 RC Makonda ameyajibu maswali hayo ambapo amesema……….

>>>’Baada ya shisha kukatazwa baadae imerudi taratibu, kila nikiuliza mbona shisha nasikia ipo, taarifa ninazopewa na jeshi la polisi ni kwamba haipo, siku moja mimi mwenyewe nimepita maeneo 10 nimekamata mwenyewe ndio maana nikasema kwa nini mnasita kuchukua hatua?, mnavyoniamba hakuna  mbona mimi mwenyewe nimekamata maeneo zaidi ya 10′

AyoTVMAGAZETI: CHADEMA yaja na amsha amsha nchi nzima, Mishahara ya vigogo yafyekwa

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement