Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Chelsea wakubali kipigo Stamford dhidi ya Liverpool

on

Baada ya usiku wa Septemba 15 2016 kuchezwa kwa mechi za ufunguzi wa michuano ya Europa League, usiku wa Septemba 16 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia mchezo wa EPL uliokuwa unawakutanisha majogoo wa jiji Liverpool dhidi ya wenyeji wao Chelsea ya London katika uwanja wao wa Stamford Bridge.

4241

Chelsea waliochini ya kocha wao Antonio Conte wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani walikubali kufungwa goli 2-1 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp, Chelsea walichukua dakika 19 kuruhusu magoli mawili yaliowafanya wakose point tatu wakiwa nyumbani, Dejan Lovren ndio alianza kupachika goli la Liverpool dakika ya 17.

4824

Wakati Chelsea wanatafakari namna ya kusawazisha Jordan Henderson akapachika goli la pili dakika ya 36, goli pekee la Chelsea lilifungwa na Diego Costa dakika ya 62, hii ni mara ya pili mfululizo kwa Chelsea kuruhusu kufungwa na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu.

tr

Msimamo wa EPL baada ya mchezo huo

October 31 2015 Liverpool walimfunga Chelsea tena goli 3-1 katika uwanja huo, mara ya mwisho Chelsea kumfunga Liverpool katika uwanja wao wa Stamford Brigde kwa mechi za Ligi Kuu ilikuwa December 29 2013 na alimfunga goli 2-1.

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement