Tangaza Hapa Ad

Mix

Mtangazaji wa TV amempa ofa Obama kwenda Kenya… Lakini kwa sharti hili

on

Akiwa amebakiza siku chache kuendelea kuitawala nchi ya Marekani kama Rais wa nchi hiyo, Barack Obama amepewa ofa ya kushangaza na mtangazaji maarufu wa radio and TV aitwaye Sean Hannity, ambaye ni rafiki wa karibu wa mgombea Urais wa chama cha Republican Donald Trump.

Mtangazaji huyo mwenye sifa kubwa ya kuendesha vipindi vya TV na Radio vinavyofatiliwa sana na watazamaji na wasikilizaji wengi ametoa ofa ya kumlipia Rais Obama gharama zote za safari ili kiongozi huyo achague sehemu yoyote ya kwenda zikiwemo Canada au Indonesia.

“Tena nitakulipia ndege binafsi ya Donald Trump kama tu utanikubalia, na utachagua sehemu au nchi yoyote unayotaka kwenda,” – Hannity 

Hannity amekuwa mtetezi mkubwa sana wa Donald Trump kupitia vipindi vyake vya TV, huku akimpiga waziwazi mgombea wa Democratic, Hillary Clinton.

han
Donald Trump akiwa na Mtangazaji Sean Hannity

Kupitia vipindi vyake Mtangazaji huyo amesema yuko tayari kumkodia Obama, ndege kubwa zaidi ya ile inayotumiwa na Rais wa Marekani, Air Force One, ila tu kwa sharti moja ambalo ni kutorudi tena Marekani akiondoka.

“Unataa kwenda Canada? Nitakulipia ili uende huko. Unataka kwenda Kenya, niko tayari kukulipia gharama zote uende Kenya. Au unataka kwenda Jakarta, sehemu ulikosoma shule, unaweza kwenda tu. Kokote unakotaka kwenda nitalipia tena kwa kuweka chakula kizuri, malazi, vinywaji, na kila kitu kitakua kina jina lako. Ila tu nina sharti moja, ukienda usirudi tena Marekani.” Hannity

Sean Hannity ni mmoja kati ya watangazaji wa TV wanaolipwa pesa nyingi sana duniani. Inaelezwa kuwa mapato yake kwa mwaka ni zaidi ya dola za Marekani Milioni 30 ambazo analipwa kupitia kipindi chake cha The Sean Hannity Show. Pia anafanya kipindi kingine cha Hannity kupitia channel ya Fox News. Kwa mujibu wa New York Times walimtaja mtangazaji huyo kama mwandishi anayeuza zaidi nchini Marekani.

ULIPITWA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO OCTOBER 27? NIMEKUWEKEA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement