Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Mwanzilishi wa REGITA na kisa cha Baba kumbaka Bintie akimtishia kumuua

on

Leo June 12, 2018 Mwanzilishi wa Taasisi ya REGITA nchini Tanzania Dainess Titompesa amezungumza na AyoTV na millardayo.com kuhusu Mwanamke anavyoweza kujisaidia mwenyewe ili ajikwamue katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kiafya.

Dainess amesema kumekuwa na wimbi kubwa la Wasichana ambao wanakumbwa na matatizo na hawajui wapi pakuanzia ndio sababu ya yeye kuanzisha Taasisi hiyo ambayo ni ya kijamii kwa lengo la kuwasaidia kuchukua hatua na hivyo kuwakutanisha Wasichana June 23, 2018 amabapo watakutana Lulu hall, Sinza Mapambano.

Katika event hiyo watakuwepo wasemaji mbalimbali pia wanasheria kwa ajili ya utoa ushauri na kuwasaidia mabinti waliotendewa vitendo viovu njia ya kujikwamua.

“Mabinti wengi wamelala, wamepoteza matumaini ya kusonga mbele kimaisha, wengi wanatamani hata kujiua na wengine wanajiuza, sisi REGITA tunataka binti ajitambue, Binti akifahamu nini kimemleta Duniani atajithamini na kuamka” Dainess

RPC “Alimtembezea kipigo hadi akazirai, asubuhi alikutwa amefariki”

 

Soma na hizi

Tupia Comments