Tangaza Hapa Ad

Michezo

Baada ya Diamond kukabidhiwa Bendera ya taifa,Ridhiwani Kikwete kayaandika haya .

on

Zikiwa zimepita saa chache toka Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Nape Nnauye amkabidhi bendera ya taifa Diamond Platnumz kwenda nayo Gabon kwenye uzinduzi wa kombe la mataifa Afrika kumekua na maoni tofauti kwa namna ilivyopokelewa hatua hiyo hasa kwenye upande wa michezo kwa nchi ya Tanzania.

Mmoja kati ya watu waliotoa maoni yao ni pamoja na Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya nne,Ridhiwani Kikwete ameandika >>‘TFF nadhani mnajua kuwa Mungu wa Watanzania anawaona. Tumefika hapa baada ya Mpira kutushinda kabisa. Sasa tunatoa Bendera kwa wanaokwenda Kuburudisha na sio wanamichezo tena…….. Ngashindwa mie’.

Post hiyo imepata zaidi ya likes 1500 na comment zaidi ya 150.

Hizi ndizo nyimbo bora za Ridhiwani Kikwete kwa mwaka 2016,Bonyeza play kuzitazama.

Tupia Comments

Advertisement