Michezo

Robert Lewandowski asaini kuichezea Bayern Munich.

on

Robert-Lewandowski

Klabu ya Bayern Munich hii leo imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski .

Lewandowski amesaini mkataba wa miaka mitano ambapo ataanza kuichezea Bayern Munich mwezi julai mwaka huu baada ya kuisha kwa msimu wa sasa wa ligi ya Ujerumani ambako atakuwa anamalizia mkataba wake na Borrusia Dortmund.

Robert Lewandowski anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya Bayern Munich baada ya kusaini ikiwa ni taratibu za mwisho kabla ya kujiunga nayo rasmi.

Lewandowski yuko kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake na Dortmund hali inayomruhusu kuingia makubaliano ya awali na klabu nyingine na atajiunga na Bayern kuanzia msimu ujao ambapo anaondoka Dortmund bure .

Tupia Comments