Tangaza Hapa Ad

Michezo

Maamuzi ya Ronaldo yanayoondoa matumaini ya kurudi Man United

on

November 7 2016 mshindi wa tuzo tatu za mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or Cristiano Ronaldo ameamua maamuzi ambayo yameondoa dalili na zile tetesi za muda mrefu kuwa inawezekana Ronaldo akarejea  Man United.

Ronaldo ameamua kusaini mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuichezea Real Madrid utakaomuweka klabuni hapo hadi 2021, mkataba wa Ronaldo wa sasa utamuwezesha kulipwa kiasi cha pound 365000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 900 kwa wiki.

3a26460600000578-3913302-image-a-9_1478526390827

Staa huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa amesaini mkataba huo na kueleza malengo yake kuwa anataka kucheza soka hadi akiwa na umri wa miaka 41 na anaamini atakuwa kafunga jumla ya magoli mengi katika maisha yake ya soka.

3a2666c300000578-3913302-image-a-12_1478526569503

Kutoka kushoto ni Rais wa Real Madrid Perez, Ronaldo na mama mzazi wa Ronaldo ‘Maria Dolores dos Santos Aveiro’

“Leo ni siku muhimu kuongeza mkataba na klabu niipendayo ni kitu muhimu sana kuongeza mkataba wa miaka mitano, lakini naomba ieleweke huu sio mkataba wangu wa mwisho nataka kuweka historia kwa kufunga magoli na kushinda mataji zaidi”

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement